Kiswahili / Swahili

Kama wazazi, na kama washawishi wa vijana , tunataka mafanikio mema ya watoto wetu . Sisi hufanya bidii ili tuwe mfano mwema, lakini wakati mwingine, bila makusudi, sisi huweza kusema mambo yanayoegamia tabia zisizo heshimisha

Mzunguko wa vurugu dhidi ya wanawake huanza na ukosefu wa heshima. Wakati tunapopuuza kwa maneno kama “wavulana watasalia kuwawavulana” au “alifanya hivyo kwa sababu anakupenda”, vijana huanza kuamini kwamba kuna sababu na hali ambazo tabia hizi mbovu zinakubalika.

Inabidi tukemee wenzetu wakati watu wanaposema ama kutenda mambo yanayowadharirishana kuwakosea wanawake heshima.

Kwa kuibadili mitazamo na mienendo yetu na kuwapa watoto wetu mawaidha kuhusu heshima, tunaweza kuyakabili maovu ya vurugu dhidi ya wanawake kabla hayajaanza.

Ili kujifunza zaidi tazama vifaa vya kampeni hapa chini.

Infographic

Infographic-Swahili-cover